Lifa hajakata tamaa, baada ya kushindwa mpango wake zaidi ya mara moja, kisa uwepo wa Salmin Zultash. Anarejea kwa mara nyingine, akiwa na mpango kabambe, uliyotokana na agano la zama lililofungwa miaka mingi sana iliyopita.
Historia ya kizazi kilichoingia agano hilo, inafunguliwa kwa upana. Viumbe hao wakiwa na ukinzani na wengine waliyotokana na agano. Maisha ya zamani yaliyojaa uhasama na ukatili wa kila namna. Mauaji yakitendeka kwa kasi kubwa pale maadui wawili wakutanapo.
Napo enzi hizo kukawa na siri ambayo ilizikwa mbali sana, wenyewe waliizika waliingia agano la kufuta kumbukumbu zao wasiikumbuke kusudi kuilinda wakiamini ni tumaini lao la baadaye. Inafikishwa kwa mtu mmoja, ambaye hajulikani ndiyo ailinde. Hilo ni agano jingine, lililopelekea mauaji makubwa kwa aliyeijua siri ile.